Ligi Kuu

Kapama: Tupo tayari

Sambaza....

Kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba wameseme wamejiandaa vyema kubeba alama tatu licha ya kucheza ugenini.

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Juma Mgunda amesema wanategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mtibwa haswa kutokana na Ligi kuelekea ukingoni.

“Ligi inaelekea ukingoni na kila timu inajipanga kuhakikisha inapata pointi tatu, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mtibwa lakini tumejipanga kupambana kupata pointi tatu,” amesema Mgunda.

Nae mchezaji kiraka Nassor Kapama akiongea kwa niaba ya wachezaji wa Simba kuelekea mchezo huo amesema wanaiheshimu Mtibwa na wanategemea mchezo mgumu lakini wapo tayari kupambana hadi mwisho.



“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo, Mtibwa ni timu nzuri na ina benchi zuri la ufundi tunaiheshimu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda, kikubwa mashabiki wetu tunawaomba mjitokeze kwa wingi.” Alisema Nasorro Kapama

Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi yake ya mwisho katika Dimba la Jamuhuri Morogoro kuelekea mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa katika Dimba la Manungu.

Sambaza....