Ligi Kuu

Kocha Simba Akiri Pengo la Inonga Bacca

Sambaza....

Licha ya kuanza na ushindi wa mabao manne ugenini na kubeba alama tatu mbele ya Mtibwa Sugar lakini kocha wa Simba ameonyesha kutofurahishwa na safu yake ya ulinzi.

Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ikishuhudia makosa ya wachezaji wake wa eneo la ulinzi na kupelekea kufungwa mabao mawili ndani ya dakika tatu na Matheo Anthony mshambuliaji wa Mtibwa Sugar.

 

Akizungumzia mchezo huo Robertinho alisema “Tunaendelea kufanya mabadiliko ya kikosi taratibu ili wachezaji wazidi kuzoeana,” alisema na kuongeza

“Tuna timu bora lakini tunapaswa kucheza kitimu. Nawapongeza wachezaji wangu kwa ushindi huu.”

Mabao mawili ya Mtibwa Sugar yameonekana kumkera Mbrazil huyo na hakusita kuonyesha kusikitishwa kwake na kumkosa beki wake kiongozi Henock Inonga.

Henock Inonga Bacca (katikati) akitolewa nje katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kupata majeraha.

“Henock alianza kuzoeana kiuchezaji na Che Fondoh Malone lakini ameumia. Tunae Kennedy Juma na Hussein Bakari wanafanya vizuri lakini wanapaswa kucheza pamoja mara kwa mara ili wawe bora zaidi,” amesema Robertinho

Inonga alipata majeraha ya bega katik mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya Singida BS Fc na hivyo anatajiwa kukaa nje wiki nne.

Eneo la ulinzi wa kati la Simba sasa lipo chini ya Che Malone, Kenedy Juma na ingizo jipya timu hiyo Hussein Kazi pia na kiraka Nassoro Kapama.

Sambaza....