ASFC

Kocha Simba: Tunaitaka Nusu Fainali.

Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba wanashuka dimbani leo kumenyana na Ihefu Fc katika  mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA maarufu kama Azamsports Federation Cup.

Kuelekea mchezo mchezo huo wa robo fainali kocha wa Simba Robert Oliveira amesema wanahitajo kucheza vizuri ili kufuzu kwenda nusu fainali mbele ya wabishi Ihefu Fc “Mbongo Maji”.

 

“Tunahitaji kucheza vizuri na kupata ushindi utakaotupeleka nusu fainali. Tunajua tunaenda kukutana na timu ngumu lakini tumejipanga.” 

“Tumetoka kucheza mechi ngumu ya Ligi ya Mabingwa lakini hii pia ni muhimu kwetu tunahitaji kucheza vizuri tukiwa na mpira na tusipokuwa nao na kupata ushindi,” amesema Robertinho Oliveira.

Simba wanashuka dimbani leo saa moja usiku katika dimba la Chamanzi Complex kuwakaribisha Ihefu katika mchezo wa nusu fainali ya FA ambapo wanahita ushindi ili kuweka matumaini yakupata kikombe msimu huu.

Tayari Azam wameshafuzu kwenda nusu fainali ya michuano hiyo na mshindi wa mchezo wa leo kati ya Simba na Ihefu  atakutana na Azam Fc.

Bingwa mtetezi wa kombe hilo Yanga Sc wao watashuka dimbani kesho katika uwanja huohuo wa Chamanzi kuvaana na Geita Gold katika robo fainali ya mwisho ya FA. Fainali ya mwaka huu itafanyika mkoani Tanga wakati michezo ya nusu fainali itafanyika Singida na Mtwara. 

Sambaza....