Robertinho Oliveira kocha mkuu wa Simba akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya Wydad Casablanca
Ligi Kuu

Kocha Simba: Tutacheza Soka la Kimataifa Kesho

Sambaza....

Ligi kuu ya NBC inaendelea tena hapo kesho katika michezo ya kwanza ya ufunguzi ambapo Simba Sc watakua wageni wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu Morogoro.

Kuelekea mchezo huo wa Ligi kocha mkuu wa klabu ya Simba Robert Oliveira amejinasibu timu yake ipo tayari na watacheza soka la kimataifa.

 

Akiongea katika mkutano na Wanahabari kuelelea mchezo huo  kocha amesema“Tunahitaji kucheza soka safi na kushinda, hilo ndilo lengo letu,” alisema na kuongeza;

“Simba ni timu kubwa na ipo juu kwenye viwango vya ubora wa Afrika, wapinzani wetu wanapaswa kutuheshimu nasi tunawaheshimu pia,” alimalizia Robertinho.

Israel Patrick Mwenda.

Nae Israel Patrick Mwenda akiongea kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema anatarajia mchezo mgumu kutoka kwa Mtibwa Sugar.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Mtibwa ni timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Tunaomba mashabiki wetu mje kwa wingi uwanjani kutupa sapoti,” amesema Israel

Baada ya kuiongoza Simba kutwaa taji lake lakwanza msimu huu mbele ya Yanga sasa kocha huyo anakibarua chakuiongoza Simba kutwaa taji  la Ligi kuu ya NBC ambalo lipo mikononi mwa Yanga.

Sambaza....