ASFC

Kocha Simba: Tutatumia wachezaji wengine kombe la FA

Sambaza....

Klabu ya Simba itashuka dimbani leo kuvaana na African Sports katika mchezo wa FA maarufu kama Azamsports Federation Cup utakaopigwa saa kumi jioni katika Uwanja wa Uhuru.

Kocha mkuu wa Simba Mbrazil Robert Oliveira amesema wamejiandaa kushinda mchezo huo ili kuendelea kupambania taji hilo na kuonyesha ukubwa wa Simba.

 

Robert Oliveira “Tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho wa ASFC dhidi ya African Sports, Simba ni timu kubwa na tunahitaji kushinda kila taji na tupo tayari.”

Mbrazil huo pia amesema kwa kiasi kikubwa watatumia wachezaji ambao wamekua hawapati nafasi katika kikosi cha kwanza kutokana na jinsi ratiba ilivyowabana.

Robert Oliveira

“Tunategemea kuwatumia wachezaji ambao hawajapata nafasi kubwa kikosini kwa kuwa tuna mchezo wa marudiano nyumbani dhidi ya Vipers kwa hiyo tunaziangalia mechi zote,” amesema Robertinho

Baada ya mchezo wa leo dhidi ya African Sports Simba itaingia tena uwanjani siku ya Jumanne March saba kuvaana na Vipers katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sambaza....