Spocha

Mastaa Simba na Yanga Wazindua Duka Sinza!

Sambaza....

Mashabiki, wadau na wapenzi wa vilabu viwili vikubwa nchini Simba na Yanga wameshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la samani maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam.

Uongozi wa duka la Mkombozi Furniture umefungua tawi lingine katika eneo la Sinza Afrikasana ambapo ufunguzi huo ulifanyika ukihudhuri wa wadau wa soka wa Simba na Yanga kama msanii Tunda Man, Jimmy Kindoki, God Yanga pamoja na Mstahiki Meya wa Dar es salaam Mh. Omar Kumbilamoto.

Mtendaji mkuu wa Mkombozi Furniture Rashidu Zakaria (katikati) akiwa na wafanyakazi wa duka hilo jipya lililopo Sinza Afrikasana.

Akizungumza mbele wa waandishi wa habari Rashidu Zakaria amewakaribisha wateja katika duka hilo jipya lililopo Sinza Afrikasana.

Tazama jinsi kina Tundaman, Mheshimiwa mstahiki Meya na wadau wengine katika hafla hiyo ilivyofanyika katika duka jipya la Sinza Afrikasana.

 


Sambaza....