Tetesi

Onyango Haendi Popote, Nabi Akiri Kusikitishwa Kukosa Kibarua

Sambaza....

Mlinzi wa kati wa Simba ataendelea kuhudumu Simba mpaka pale mkataba wake utakapomalizika na hakuna barua aliyoipeleka kusitisha mkataba amesema Ahmed Ally [Sport Xtra]

Makamu wa rais wa Yanga amewahakikishia Wanachi mshambuliaji Fiston Mayele hatokwenda popote licha ya kutakiwa na vilabu vya Uarabuni [Sport Xtra]

Kevin Kijiri mlinzi wa kulia wa KMC huenda msimu ujao akahamia Singida Fountaine Gate baada ya klabu hiyo kuonyesha kuhitaji huduma yake [Mwanaspoti]

Nickson Kibabage

Mlinzi wa kushoto wa Singida Fountaine Nickson Kibabage yupo katika hatua nzuri ya kuhamia klabu ya Yanga baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana uhamisho huo. [Mwanaspoti]

KAMA mambo yataenda sawa, Mbrazili Caique Luiz Santos da Purificacao (25), muda wowote kuanzia sasa anaweza kutua aridhi ya Tanzania na kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba [Mwanaspoti]

Kambi ya Nasraddine Nabi imethibisha kusikitishwa na kitendo cha Kazier Chiefs kumtangaza kocha mpya licha ya kukaa katika makubaliano kwa muda mrefu [Kickoffs]

Sadio Kanoute “Putin”

Kiungo wa Simba Sadio Kanoute amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Simba baada ya ule wa awali kumalizika.

Wilfried Zaha atakuwa mchezaji huru siku ya Ijumaa, lakini fowadi huyo wa Ivory Coast, 30, bado yuko kwenye mazungumzo na Crystal Palace ili akubali mkataba mpya. [Mail]

Meneja wa Roma Jose Mourinho anatazamia kumnunua mshambuliaji wa Leicester City wa Nigeria Kelechi Iheanacho, 26, na fowadi wa Zambia Patson Daka, 24. [Express]

Patson Daka

Simba imeongeza dau mpaka dola 70,000 ili kumpata mlinzi wa Cotton Sports, Che Fonde Malone ambae tayari wameshakubaliana maslahi binafsi, mlinzi huyo atasaini mkataba wa miaka mitatu [Nuhu Adams]

 

 

Sambaza....