Mchezo wa mwisho wa kundi hilo Yanga watamalizia ugenini Congo dhidi ya Mazembe hivyo ni vyema leo wakamalizana na Monastir wakiwa nyumbani Kwa Mkapa na kufuzu robo fainali.
Na tayari muitikio mkubwa umeonekana huku baadhi ya mashirika na watu binafsi wakinunua tiketi 100 mpaka 300 kwa wakati mmoja ilo zigawiwe kwa wanawake wataokwenda katika mchezo huo.
Yanga wanahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi yakufuzu robo fainali kwani kusuasua kwa Mazembe kumezidi kuwapa nafasi katika kundi hilo ambalo US Monastir anaonekana ndio mbabe
Kwa hesabu zozote zile leo Yanga hawapaswi kupoteza mchezo kama itashindikana alama tatu basi angalau wapate alama moja ili kuendelea kuweka hai matumaini yao ya kufuzu robo fainalo