Shirikisho Afrika

Yanga: Real Bamako watakwenda kutoa ushuhuda kwao.

Sambaza....

Klabu ya Yanga leo mchana imeongea na mashabiki wao kuelekea mchezo wao wanne wa kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa wiki ijayo.

Kupitia msemaji wao Alli Kamwe wamesema wanataka mashabiki wa Yanga ndio waamue mechi hiyo kwa jinsi ambavyo watashangilia lakini pia Yanga wametangaza kauli mbiu yao watakayokwenda nayo katika mchezo huo.

 

“Kauli mbiu yetu kuelekea mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Real Bamako ni siku ya Jumatano March nane ni “Kwa Mkapa Full Shangwe,” alisema Alli Kamwe

Kamwe pia amesema wanataka Real Bamako wakirudi kwao Mali watoe ushuhuda kwa walichokiona kwa Mkapa kutoka kwa mashabiki wa Yanga.

Mashabiki wa Yanga

Ali Kamwe “Tunataka Bamako wakiondoka kwenda kwao Mali wawaambie watu wakwao wamekutana na klabu yenye mashabiki bora kabisa barani Afrika.”

Yanga wanahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi yakufuzu robo fainali kwani kusuasua kwa Mazembe kumezidi kuwapa nafasi katika kundi hilo ambalo US Monastir anaonekana ndio mbabe.

Sambaza....