Fiston Kalala Mayelle akishangilia bao lake dhidi ya Real Bamako
Shirikisho Afrika

Yanga sio kinyonge wabeba alama ugenini

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kupata alama moja katika mchezo wao watatu wa kundi D katika kombe la Shirikisho  barani Afrika mbele ya wenyeji wao Real Bamako.

Yanga walikua ugenini katika Dimba la Mars 26 wakicheza na vibonde wa kundi lao Real Bamako ya nchini Mali. Katika mchezo ambao Yanga waliutawala kwa kiasi kikubwa na kama wangekua makini zaidi huenda wangendoka na alama tatu.

 

Yanga ndio waliokua wakwanza kupata goli kupitia kwa Fiston Kalala Mayele aliepiga shuti kali la chini baada ya kuwahadaa mabeki wa Bamako kwa kugeuka kwa haraka na kulitazama lango lao kisha kufumua shuti kali.

Yanga watapaswa wajilaumu wenyewe kwakukosa alama zote tatu kwani waliruhusu bao dakika za mwisho za mchezo huku likifungwa kwa aina ileile ya mpira uliokufa. 

Baada ya mchezo huo sasa Yanga inafikisha alama nne nakuendelea kukaa katika nafasi yake yapili nyuma ya US Monastir wenye alama saba.

Msimamo wa Kundi D.

Awali kabla ya mchezo huo katika kundi D ulipigwa mchezo wa mapema ambapo TP Mazembe walikubalo kipigo cha mabao mawili kwa bila wakiwa nyumbani dhidi ya US Monastir

Sambaza....