Stori

Uongozi Simba Waomba Radhi kwa Mashabiki Wao

Sambaza....

Mwenyekiti wa Bodi wa Klabu ya Simba Salim Abdallah maarufu kama Try Again amewaomba msamaha mashabiki na wapenzi wa klabu ya Simba kutokana na muenendo mbovu wa timu yao msimu huu.

Mpaka sasa Simba wanauhakika wakutoka kapa msimu huu bila kupata kikombe chochote kutokana na kutolewa katika michuano yote huku katika Ligi wakichzeza kukamilisha ratiba tuu. 

Akizungumzia msimu huu ulivyo kwa Wanasimba Salim Abdallah amesema “Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi nachukua nafasi hii kuwaomba radhi Wanasimba wote, hatukuwa na msimu mzuri sababu tumekosa mataji yote.

Wachezaji wa Simba wakati wa upigani mikwaju ya penati katika mchezo dhidi ya Wydad Casablanca

“Tumekuwa na changamoto ya majeruhi kikosini, wale tuliowaongeza pia wameshindwa kuonyesha ubora lakini ndio mpira tunajipanga kwa msimu mpya.” 

Tumaini pekee la Simba lilikua ni kombe la FA kabla ya kufungwa na Azam Fc katika nusu fainali na hivyo kuhitimisha msimu wakiwa bila kikombe kwani walishakosa kombe la Mapinduzi, wakaondoshwa Ligi ya Mabingwa robo fainali na katika Ligi Yanga yupo katika nafasi nzuri yakutwaa ubingwa huo.

 Simba sasa wanakwenda msimu wapili mfululizo bila kutwaa kikombe chochote kikubwa na hivyo  kuendelea kuipa nafasi Yanga kuendelea kutawala na kubeba vikombe katika Ligi na Kombe la FA.

Sambaza....