Stori

Bado Simba Wana Nafasi Yakutimiza Ndoto Yake!

Sambaza....

Ally Salim ni golikipa mwenye umri mdogo sana ambaye anahitaji kukomaa zaidi kupitia Simba SC ambao wamempa nafasi kwenye michezo kadhaa mikubwa.

Simba kama klabu pamoja na Tanzania kwa ujumla kama nchini itanufaika sana na Ally Salim kwanza ubora wake, pili umri wake bado mdogo sana.

 

Nafasi ya kujifunza kwake ipo siku zote kuanzia kwa kina Aisha Manula, Beno Kakolanya na Ally Mustapha huku pote amepata darasa zuri.

Ni karata ngumu sana kwa Simba kucheza karata hii ya Ally Salim! Narudia ni ngumu sana kwa sababu mbele kuna mechi na mashindano yenye presha kubwa sana katika eneo analocheza.

Mechi ya Wydad Casablanca alicheza vizuri sana! Mechi ya Kariakoo akapewa nafasi na kila kitu kilikuwa boa zaidi ndani. Hii Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans naona akipata nafasi pia.

Ally Salim akiokoa mkwaju wa penati wa penati katika katika mchezo wa Ngao ya hisani dhidi ya Singida Fountaine Gate Fc.

Salim anahitaji hizi mechi kubwa ili kukomaa zaidi ijapo ni ngumu Simba kucheza karata hii sababu bado wana uoga dhidi yake ameachwa mbali sana kwa ubora dhidi ya Aishi Manula.

Pale Man United walikuwa na Dean Henderson ambaye pia alipitia wakati mgumu dhidi ya David de Gea kama ilivyo kwa Ally Salim hivi sasa mbele ya Aishi Manula.

Ni ngumu kumuamini moja kwa moja Ally Salim ijapo Simba hawatakiwi kumpoteza sababu ni moja kati ya wachezaji vijana ambao wana ubora na yimu inahitaji mikono yake eneo la golini.

Rahisi! Ngao ya Jamii siku ya kesho dhidi ya Young Africans naona Ally Salim akipata nafasi golini.

 

Sambaza....