Che Fonde Malone
Uhamisho

Beki Simba Aweka Rekodi ya Usajili Cameroon

Sambaza....

Baada ya kukamilisha uhamisho wake akijiunga na Simba akitokea Cotton Sports ya Cameroon Che Fondoh MaloneChe Fondoh Malone ameingia katika rekodi ya usajili ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Kick442 Simba  wametoa dola 130,000 kwa Cotton Sports ili kukamilisha usajili wa mlinzi huyo wa kati na kumfanya beki ghali katika historia ya klabu hiyo ya Cameroon.

Malone amesaini mkataba wa miaka miwili ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi alitua nchini  Jumamosi na kupima afya na baadae kutambulishwa rasmi na Wekundu wa Msimbazi.

Mlinzi wa kati Che Fonde Malone akitambulishwa Simba Sc.

Nyota huyo mwenye miaka 24 tayari ameshaitwa timu ya Taifa ya Cameroon mara tano ikiwa ana uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kulia pia.

Name
Che Fondoh Malone
Utaifa
cmrCameroon
Nafasi
Mlinzi
Urefu
1.8
Sasa
Simba SC
Ligi
Ngao ya Jamii, TPL
Misimu
2023-2024

Malone pia ni mchezaji bora wa Ligi ya Cameroon akitoka kutwaa tuzo hiyo Ijumaa ya wiki iliyopita anaejulikana kwa jina la utani “Ukuta we Jeriko” anakwenda kuungana na Kenedy Juma, Nasoro Kapama na Inonga Baka katika eneo la mlinzi wa kati.

Sasa Malone anakwenda kuungana na Mcameroon mwenzake Willy Onana katika klabu ya Simba ambao hivi karibuni watakwenda nchini Uturuki kwa maandalizi ya msimu ujao. 

 

[poll id=”10″]

Sambaza....