Benno Kakolanya
Tetesi

Benno Kakolanya Huyoo Singida Big Stars

Sambaza....

Mlinda mlango namba mbili wa klabu ya Simba Benno Kakolanya msimu ujao anatarajia kuachana na Wekundu wa Msimbazi Simba na kutimkia kwa walima alizeti Singida Big Stars.

Benno Kakolanya ambae amedumu na Simba takribani misimu minne tangu ajiunge nao akitokea kwa mahasimu wao Yanga  amekua akionyesha kiwango kizuri pindi anapopata nafasi licha ya kukaa muda mrefu benchi akimtazama kipa namba moja wa Simba Aishi Manula akiwa langoni.

 

Mchezaji huyo wa zamani wa Tanzania Prisons inasemekana ameshamalizana na Singida Big Stars kwa kusaini mkataba kwani tayari mkataba wake na Simba unaelekea ukingoni ukiwa umebakiza miezi michache umalizike.

Licha ya kuhitajika na Simba chini ya Mtendaji mpya Imani Kajula ambae alikua tayari katika mazungumzo ya kumuongezea mkataba lakini Benno ameonekana kuchanganywa na dau nono alilowekewa na Singida Big Stars na hivyo kupelekea kukubali kuachana na Simba.

Beno Kakolanya akinyaka mpira katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini dhidi ya El-Merreck ya Sudan

Big Stars wamekua na kiu yakuwakilisha nchi Kimataifa na mpaka sasa wapo nafasi ya tatu kwenye Ligi lakini pia wapo nusu fainali ya michuano ya FA ambayo wanaweza kukata tiketi ya kuwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika. Hivyo wameanza kutengeneza kikosi bora na chenye ushindani wakitaka kuongeza wachezaji wenye uzoefu.

Ni wazi sasa Simba imepata pigo na watapaswa kuingia sokoni kutafuta mlinda mlango namba mbili mweye uwezo mkubwa ambae atakua tayari kumpa changamoto Aishi Manula.

 

Sambaza....