AFCON

Clatous Chama Akubali Yaishe kwa Kocha wa Chelsea

Sambaza....

Kiungo wa Chipolopolo Clatous Chota Chama anasema amefurahishwa na kufuzu kwa timu hiyo kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2023. Chama, ama Triple C amefuta uvumi kwamba hakufurahishwa na uamuzi wa Kocha Avram Grant wa kumweka kwenye benchi wakati wa ushindi dhidi ya Ivory Coast Jumamosi.

Mwamba wa Lusaka alikuwa akizungumza kwenye Facebook moja kwa moja “live”. Mchezaji huyo wa Simba SC alisema yuko sawa na uamuzi wa Grant na amefurahishwa na jinsi wachezaji waliochaguliwa walivyocheza.

Kiungo huyo wa zamani wa ZESCO United anasema ni lazima tu awe tayari kwa nafasi yake na ana imani itakuja. “Mimi niko sawa na uamuzi wa kocha, tunacheza soka kwa ajili ya taifa si binafsi, wachezaji waliocheza, walifanya vizuri, unadhani unategemea kocha hafanyi mabadiliko kutokana na jinsi mchezo ulivyokuwa ukiendelea,” alisema. 

“Nimefurahishwa na wachezaji waliocheza, uamuzi wa kocha, mashabiki waliokuja kuunga mkono, na nina furaha sana kwamba tumefuzu. Je, ningeingia na kufanya makosa halafu tukapoteza mchezo au sare? Mashabiki wangesema nini? “Lazima uwe tayari kwa nafasi yako na nina uhakika itakuja na nitakuwa tayari kwa hiyo,” aliongeza.

Bao la Patson Daka na Klings Kangwa pamoja na Serge Aurier la kujifunga liliwapa Chipolopolo ushindi mnono kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa Jumamosi na kujihakikishia kufuzu kwa pambano hilo la bara.

Avram Grants kocha wa zamani wa Chelsea atakua ameipeleka Zambia Afcon kwa mara ya 18  na ni kwa mara ya kwanza kwa Zambia kucheza tangu mwaka 2015. 


Sambaza....