Ligi Kuu

Jean Baleke aongeza msiba Manungu

Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kupata ushindi muhimu katika kiwanja kigumu ugenini Manungu Complex katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Simba wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri na kubeba alama zote tatu mbele ya wenyeji wao Mtibwa Sugar ambao wameshika dimbani kwa mara ya kwanza tangu walipofiwa na mlinzi wao wa kati Idd Mobby Mfaume.

Ni Jeab Baleke ndio alipeleka huzuni kwa Mtibwa Sugar baada ya kufunga mabao matatu tena katika kipindi cha kwanza cha mchezo. Baleke alifunga magoli katika dakika ya tatu, saba na thelathini na nne  ya mchezo.

Kwa kufunga mabao hayo matatu “hatrick” anaungana na John Bocco, Fiston Mayele na Ibrahim Mukoko msimu huu ambao nao wamefunga hatrick na kufanya zifike tano msimu huu.

Jean Balake akipiga mpira na akifunga mbele ya mlinzi wa Mtibwa Sugar

Kwa ushindi huo sasa Simba wanafikisha alama 57 nyuma ya Yanga wenye alama 62 kileleni mwa Ligi. Yanga wanashuka dimbani tena kesho kumenyana na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC. 

Sambaza....