Zamani

Jinsi Simba Walivyopeleka Maafa Zambia Mwaka 1979

Sambaza....

Wakati Mufulira Wanderers Wanashinda ubingwa wa ligi mwaka 1978, ilikuwa ndiyo mafanikio yao ya mwisho kwa karibu miaka 20 iliyofuatia. Wakiwa kama Mabingwa wa Zambia, Wanderers waliiwakilisha Zambia katika mashindano ya Kombe la Vilabu la Afrika mwaka 1979.

Baada ya kuifunga Simba ya Tanzania magoli 4–0 mjini Dar es Salaam katika mchezo wa raundi ya kwanza, Wanderers waliwakaribisha Simba kutoka Tanzania katika mechi ya marudiano mnamo April 1 mwaka 1979 mjini Lusaka, katika mechi ambayo ilionekana ni ya kukamiliisha ratiba tu.

Mechi hiyo ilikuja kugeuka maafa wakati Wanderers walipochabangwa magoli 5–0 na kutupwa nje ya mashindano kwa jumla ya tofauti ya magoli 4–5 na kufuta ule ushindi wao wa Dar es salaam.

Magazeti ya Zambia yakiandika kuhusu mechi hiyo waliita kuwa “mechi ya matokeo mabaya kabisa kuwahi kutokea kwa Wanderers katika historia” na kwamba ni “Jambo kubwa kabisa katika sikukuu ya wajinga duniani,” (“most miserable performance in history” and “a big April Fool’s Day affair.”)

Sambaza....