Keneth Muguna.
Uhamisho

Kiungo Aaga Mapema Azam Fc Atimkia Kwao

Sambaza....

Kiungo Kenneth Muguna ametangaza kuachana na Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika taarifa yake, Muguna alielezea shukrani zake kwa muda wake katika klabu hiyo.

Muguna ambaye ni kiungo mahiri alitoa taarifa za kuondoka kwake Azam FC na kueleza kuwa ilikuwa ni jambo mkubwa katika kipindi chake cha miaka miwili akiwa na klabu hiyo.

Kiungo huyo wa kati wa Harambee Stars aliiaga klabu hiyo na kuelezea kuthamini kwake fursa na kumbukumbu alizozipata akiwa huko. “Ilikuwa uzoefu mzuri, nilifurahia miaka hiyo 2 #AdiosAzam,” Muguna alisema katika taarifa yake.

Keneth Muguna wa Azam Fc akipambana na kiungo wa Polisi Tanzania Tariq Simba

Kuondoka kwa kiungo huyo kutoka Azam FC kunaashiria mwisho wa historia kubwa katika maisha yake ya soka, na kunafungua uwezekano wa safari yake ya soka katika klabu nyingine.

Muguna alijiunga na Azam Fc miaka miwili iliyopita akitokea kwa wababe wa Kenya Gor Mahia huku pia akiitumikia timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars. Majeruhi na ushindani mkubwa wa namba ni kwa kiasi kikubwa ndio vimepeleka kutokufanya vyema na kukosa nafasi ya kikosi cha kwanza Azam Fc.

Sambaza....