Sambaza....

Azam FC ndio tunahesabu kama wapinzani wa Yanga na Simba kwenye Ligi kuu ya Tanzania tangu wachukue ubingwa huo mwaka 2014 lakini kwao imekuwa tofauti sana.

Miongoni mwa klabu chache za Tanzania zilizokamilika kwenye miondombinu ya michezo basi Azam FC huwacha acha kutaja jina lao, tena unaweza kukuta wao ndio wanaongoza au wapo peke yao tu.

 

Miaka ya hivi karibuni wamesajili wachezaji wengi wazuri sana hasa wa kimataifa na imeonekana kuwa kwa wafuatiliaji wengi wa soka Tanzania wamekili mara kadhaa kuwa Azam wanaenda kugombania ubingwa lakini imekuwa tofauti kwao kuanzia msimu jana kurudi nyuma.

Msimu huu wameanza vizuri kwa kushinda mechi 3 mfululizo ambazo zilifanya watu kuona msimu huu huenda wakatoa upinzani mkubwa sana kwa Simba na Yanga ijapo kwa mchezo wa jana wamepata alama moja ambayo sio mbaya lakini inapunguza kitu dhidi ya wapinzani wao.

Feisal Salum akitambulishwa rasmi na Azam Fc.

Ndani ya klabu wamefanya usajili wa wachezaji wazuri kama Feisal Salum, Yanick Bangala, Yahya Sidibe na wengine wengi hapo bado kuna ambao wapo ndani ya timu tangu msimu uliopita kama Kipre JR, Idd Nado, Sospeter Bajana, James Akaminko.

Baada ya kutoka sare jana dhidi ya Dodoma Jiji hii imewapa tahadhari tu sababu msimu uliopita mechi zilizowapa ugumu kwenda kushindania ubingwa dhidi ya Simba na Yanga kwenye basi ni hizi za ugenini ambazo waliacha alama mbele ya timu za kati.

Mshambuliaji wa Dodoma Jiji akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa Azam Fc Daniel Amoah.

Kwa mfano msimu uliopita kwenye mechi tano za mwanzo walitoa sare dhidi ya Geita Gold na kupoteza dhidi ya TZ Prisons achilia mbali sare dhidi ya Yanga ambayo ilifanya kuwa na alama 8 kwenye mechi 5 japokuwa msimu huu wana alama 10 kwenye mechi 4.

Bado wana timu nzuri ambayo naipa asilimia nyingi tu za kuchukua ubingwa msimu huu iwapo tu watashinda mechi nyingi dhidi ya hizi timu ambazo mara nyingi wameacha alama mbele yao hasa mechi ambazo wanacheza ugenini hofu yangu ni hapo tu.

Ni mwanzo mzuri kwao tofauti na msimu uliopita, hivyo bado Youssouf Dabo na Bruno Ferry wana kazi ya kufanya ili kuwalipa Azam FC kitu bora ndani ya uwanja kupitia wachezaji waliopo kwenye kikosi chao msimu huu.

 

Sambaza....