Pablo Franco
ASFC

Kocha Pablo kushusha kikosi kamili.

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa robo fainali wa kombe la Azamsports Federation Cup maarufu kama kombe la FA kocha mkuu wa Simba amesema atashusha kikosi chake kamili kuwakabili Pamba Fc.

Pablo Franco kocha mkuu wa Simba amesema katika michuano hii kwa hatua iliyofikia hakuna timu raisi hivyo atapanga wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza.

“Katika michuano hii hakuna timu rahisi, huu ni mchezo muhimu kwetu tunahitaji kushinda ili kusonga mbele. Tutapanga kikosi kamili kwa wachezaji wote waliokua tayari kwaajili ya mchezo,” Pablo Franco.

Simba wanakutana na Wana TP Lindanda  Pamba Fc katika mchezo wa robo fainali wa kombe la FA ambapo mshindi atakwenda kukutana na Yanga nusu fainali.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.