Ligi Kuu

Rekodi ngumu aliyoiweka Baleke baada ya kufunga “hatrick”.

Sambaza....

Mshamuliaji wa klabu ya Simba raia wa Congo DR Jean Baleke alifanikiwa kufunga mabao mabao matatu pekeyake yaani hatrick katika mchezo wa Ligi Kuu ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mchezo ambao Simba hawakutarajiwa kupata matokeo mazuri kutokana na ugumu wa klabu ya Mtibwa na historia mbaya kwa Simba katika uwanja wa Manungu lakini mambo yalikua tofauti na Mcongo huyo akaiteka show nzima.

 

Baleke alianza kufunga katika dakika ya tatu ya mchezo kwa pasi ya kichwa ya Moses Phiri baada ya gonga nyingi za wachezaji wa Simba. Akafunga bao la pili kwa pasi ya Saidoo Ntibazonkiza katika dakika ya nane kupitia kwa koni fupi waliyoanziana Chama na Saidoo.

Goli la tatu Baleke alilifunga katika dakika ya 34 kwa kupata pasi ya kichwa kutoka kwa Shomary Kapombe baada ya kuunganisha mpira wa juu uliopigwa na Sadio Kanoute “Putin”.

Jean Baleke akikabidhiwa mpira wake na mwamuzi Deonisia Rukya baada ya kufunga hatrick.

Kwa maana hiyo Jean Baleke ametumia dakika 29 pekee kuweza kufunga mabao matatu na kutumia muda mchache zaidi. Lakini pia katika msimu huu Baleke amefanikiwa kufunga hatrick ndani ya kipindi cha kwanza pekee.

Baada ya magoli hayo matatu sasa Baleke anaungana na nyota wengine watatu waliofunga hatrick msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC.

Baada ya kufunga magoli hayo Baleke hakufucha kuonyesha hisia zake akisema amefurani kutimiza kazi yake.

“Nina furaha kufunga hat trick ya kwanza nikiwa na Simba. Mimi ni mshambuliaji kazi yangu ni kufunga kwahiyo nawaahidi nitaendelea kufunga,” amesema Baleke.

John Bocco

John Bocco wa Simba aliefunga hatrick mara mbili, Fiston Mayele wa Yanga na Ibrahim Mukoko wa Namungo. 

Kwa magoli hayo matatu sasa Jean Baleke aliyejiunga na Simba katika dirisha dogo January hii amefikisha mabao matano katika Ligi Kuu ya NBC kwenye orodha ya wafungaji bora. 

Simba sasa wamemaliza kibarua cha Ligi Kuu Bara kwa mwezi huu wa tatu na kituo kinachofuata na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya utakaopigwa Jumamosi hii Benjamin Mkapa

Sambaza....