Mabingwa Afrika

Simba ilivyo mbovu mpaka nje ya uwanja!

Sambaza....

Zipo tabia za baadhi ya wazazi kuwatetea watoto wao kwa tabia ambazo pengine sio nzuri kwa jamii, udokozi, uhuni, uteja nk pale mzazi anapopelekewa taarifa za mtoto yule huwa mkali na kudai mtoto anaonewa bila kujali hamtengenezi ila anamharibu, madhara ya jambo hilo yanapokuja kuonekana huwa yamefika hatua ambayo mara nyingi huwa ni ngumu kudhibitika.

Juzi nilipoandika kuwa Simba kama watajitahidi sana basi watapata angalau sare, nilikua najua nini naongea kwa sasa Simba ni kama mtoto mwenye tabia mbaya ambazo hazifai kwa jamii na kila wakitaka kuambiwa ukweli wapo watu wanatetea wakidhani wanajenga kumbe wanabomoa. Zipo sehemu kuu tatu ambazo kama Simba watazifanyia kazi basi watafanya vizuri msimu ujao, maana msimu huu hamna tena hawaambulii kitu hata vikombe vya ndani sidhani kama watabeba labda kwa njia za kisela kisela.

Sehemu ya kwanza: Ubovu wa usajili.

Katika uongozi wapo pale kupiga dili tu kuanzia kwa MO mwenyewe mpaka kwa Asha baraka kwa sasa hawaangalii Simba kufanya vizuri bali wao wanafaidikaje, wanashindwa kusajili wachezaji wazuri kwa pesa za kawaida ambazo tunaotaka kushindana nao hao wachezaji wanawaweka benchi.

Luis Miquissone ambaye kwetu ni lulu mpaka leo kule Al ahly ameshindwa na mpaka leo nina uhakika haijui kesho yake sasa kama mchezaji wako tegemezi ukimuuza kwa mtu unaetegemea kukutana nae unafikira nini? Simba walishindwa kumsajili Manzoki kisa milioni 400 serious? Timu inayotaka Nusu fainali ya Africa haimuwezi mchezaji wa Milioni 400 itafikaje huko nusu, hizi fluku sio ubora huwezi tegemea bahati kila siku.

Walishindwa kusamjili Adebayo kwa kushindwa kutoa milioni 600 na mshahara wa zaid ya milioni 50 Berkane wakamchukua kwa pesa hizo na anakula mkeka huko, tunajiona wapi ukitazama hiyo mifano?

Victorian Adebayor

Kwa utafiti mdogo niliyoufanya vile vilabu kutoka Uarabuni mchezaji mdogo kabisa katika kikosi chao anaweza kuwa analipwa Milioni 50 sasa timu hii huwezi kupambana nayo zaidi kama utachomoka, utachomoka kwa bahati bahati tu.

Sehemu ya pili: Wachezaji waliopo.

Ukitaka kujua kuwa hata wachezaji waliopo kwa sasa ni wakawaida angalia wanavopata shida wakikutana na timu nzuri, Simba wanavofungwa na Yanga na Azam sio bahati mbaya, sio hujuma ila ina wachezaji wa uwezo wakawaida kiushindani. Tuache propaganda wachezaji kadha wa kadha hata wakienda Singida hawawezi kucheza sasa pale Simba wanafanya nini? 

Eneo la tatu: Utawala.

Hili linaingia kwenye uongozi tena, yule Mangungu kama alikua na hela ya kumkatia tiketi Manzoki aje Tanzania katika kampeni za uchaguzi (😂 kituko) alishindwa nini hiyo hela kuongezea wakamsajili mwaka jana zilipotakisa milioni 400 kumpataka Manzoki?

Sasa hizi siasa ndo zinaharibu soka letu haya ndio mambo ya kukemea na sio kuchekea chekea. Klabu kubwa kama Simba wanyang’anywe basi kwasababu yakushindwa kutimiza maswala yakimkataba, mara klabu kubwa kama Simba wanazindua jezi halafu bado hazijafika kwa visingizio visivyo na maana, unaweza kuona ni jinsi gani eneo la utawala la Simba ni bure bure kabisa.

Simba isijiendeshe kimazoea mbona hivi vitu havijitahiji mganga wala elimu ya unajimu kujua kuwa havipo sawa, kwani wanaoona vipo sawa wanatazama kwa jicho gani??.

Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu.

Mwisho!

Simba ikirekebisha maeneo hayo matatu kwa mtandao waliyokwisha tengeneza kule CAF nusu fainali kwao itakua kama kucheza na Ruvu shooting kila siku. 

Wasajili wachezaji wenye gharama na uwezo zaidi ya watano yaaani Chama ndo awe mchezaji mwenye kiwango kidogo kuliko watakao kuwepo.

Wasipeana uongozi kisela ila wanachama wajue timu inataka nini na nani atawafikisha, ila kwa aina ya huyu mwenyeki wao watashikana sana uchawi.

Mzamiru Yasin (katikati) akiwatambuka wachezaji wa Raja Casablanca

Watimue wale wachezaji wa kawaida baadhi wabaki nao wachache (maana robo tatu ya team wao ndo wamejaa) halafu utaniambia kama Simba haijatoboa.

Celestine Chomola [Instagram Cubic Chomox]

Sambaza....