Mabingwa Afrika

Simba Yaanza Kukusanya Mamilioni Baada ya Ushindi

Sambaza....

Kufuatia kufuzu na kwenda robo fainali kwa klabu ya Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika Wekundu hao wa Msimbazi wamefanikiwa kupata milioni mia moja za Kitanzania kutoka kwa wadhamini wao.

Simba imepokea milioni 100 kutoka wadhamini wao wakuu M-bet kama bonus baada ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo wamesema wametoa kiasi hicho cha pesa na bado pesa zipo nyingi ni Simba tu waendee kufanya vizuri.

“Mwaka jana wakati tunasaini mkataba moja ya kipengele ni kutoa bonus kwa kila hatua wanayofika kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuanzia hatua ya makundi. Leo tunatoa Tsh. 100 milioni na tunawambia tu kuna zingine zitakuja.” Allan Mushi 

Nae Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Imani Kajula amewashukuru wadhamini wao kwa kuwashika mkono na kutimiza sehemu ya mkataba wao.

Imani Kajula, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Sc

“Tunawashukuru wadhamini wetu M-Bet kwa ushirikiano ambao wanatupatia. Leo watatukabidhi kishika mkono kwa kuingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Mtendaji Mkuu Imani Kajula.

Pia katika hatua nyingine Mtendaji huyo amewaita mashabiki wa Simba uwanjani kuelekea mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Wydad Casablanca.

Imani Kajula “Mechi itachezwa siku yenye baraka, naomba kuwakaribisha Watanzania wote kuja kuangalia timu mbili bora zikicheza,” alisema na kuongeza

“Lengo letu ni kuwa klabu ya michezo bora barani Afrika. Tunaendelea kuboresha hilo kwa kuwa moja ya timu bora 10 Afrika na ndio timu pekee Tanzania ambayo itacheza CAF Super League.”

Sambaza....