Marumo Gallants
Shirikisho Afrika

Yanga Wakiri Ugumu wa Wasauzi, Waja na Slogan ya Mchezo Yamaangamizi.

Sambaza....

Wananchi Yanga baada yakuandika historia yakutinga hatua ya nusu fainali katika michuano ya Afrika sasa wanakibarua kigumu mbele ya Waafrika Kusini “Wajukuu wa Mandela” Marumo Gallants.

Tayari kuelekea mchezo huo msemaji wa klabu ya Yanga Alli Kamwe amezindua slogan wataiayoitumia kuelekea mchezo hui utakaopigwa Benjamin Mkapa siku ya Jumatano jioni.

“Tunayo slogan yetu tayari kuelekea katika mchezo huu wa nusu fainali dhidi ya Marumo Gallants ambayo iliamuliwa baada yakukaa vikao vingi sana na uongozi,” alisema Alli na kuongeza  “Slogan yetu ni “Our Team Our Time” yaani  “Timu yetu wakati wetu”. Ni wakati wetu sisi Yanga kupeperusha bendera ya nchi yetu na pia ukanda huu wa CECAFA maana sisi ndio wawakilishi pekee.”

Marumo Gallants

Kamwe pia amesema hawawezi kuidharau hata kidogo Marumo Gallants kutokana na nafasi yao katika Ligi nchini mwao  kwani kupata sare ugenini na kuwatoa Pyramids sio jambo dogo.

“Hawa Marumo Gallants sio watu wazuri  kabisa, huku Shirikisho asikidanganye mtu eti kuna timu rahisi, huku hakuna timu rahisi. Marumo walipata sare pale Misri tena dhdi ya Pyramids hili sio jambo dogo,” alimalizia Alli Kamwe

Wananchi Yanga wanatafuta nafasi adhimu yakucheza fainali ya michuano ya Afrika hivyo ni Marumo Gallants pekee wamebaki kama kikwazo kwa Yanga kufikia ndoto yao.

Sambaza....