Miaka 30 imepita tangu nchi hii ikaribie kubeba kombe la Afrika, mara ya mwisho ilikua ni 1993 sasa fikiria nchi imekaa muda wote huo bila kufika fainali.
Wananchi Yanga wanatafuta nafasi adhimu yakucheza fainali ya michuano ya Afrika hivyo ni Marumo Gallants pekee wamebaki kama kikwazo kwa Yanga kufikia ndoto yao.
Kuelekea mchezo huo Alli Kamwe ametangaza viingilio vitakavyotumika pamoja na muda wa mchezo utakaochezwa huku ukitoka kuchezeka usiku na sasa utapigwa jioni.
Kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari mechi hiyo iliandaliwa ili kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya Silent Ocean Ltd na Waandishi wa Habari za Michezo.
Katika zoezi hilo alikuepo Afisa habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe ambae hakusita kuwaita Wananchi siku ya Jumapili ili kuwashangilia wachezaji wao na kuiteketeza TP Mazembe.