Abdul Mkeyenge

Mchambuzi
Mwandishi wa gazeti la Raia Mwema. Hapa anaandika makala za mpira wa ndani na nje.
Ligi KuuUhamisho

Mgosi ‘again’? Naweka karata yangu kwake

MUSSA Hassan Mussa Mgosi amerudi tena uwanjani baada ya miezi kadhaa kujitokeza uwanja Taifa kulikokuwa kumetamalaki mashabiki wa Simba na kuchukua kipaza sauti na kusema ameamua kustahafu soka. Japo nilikuwa mbali na Mgosi alipokuwa akizungumza maneno yale, lakini alionekana kama mtu aliyestahafishwa sio kustahafu kwa matakwa yake. Alitoa chozi la...
EPL

Moses amedhulumiwa jasho lake

NAPAZA sauti juu yangu nikisema wazi Victor Moses amedhulumiwa jasho lake. Nitasema hivi kokote kule ambako nitaitwa kuelezea amedhulumiwaje. Nitakueleza huko chini. Shusha pumzi kwanza. Haya ipandishe tuendelee. Jina la Moses haliko katika tatu bora ya wachezaji wa Afrika wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka huu. Majina yaliyoko ni...
Mashindano

Heroes wametupa maana ya kuvaa jezi ya taifa

JANA jioni Zanzibar Heroes wamekufa kiume katika ardhi ya Mzee Jomo Kenyata pale Kenya. Wamekufa kiume kwa mapigo ya penati. Mapigo ya penati hayajawahi kuwa na mwenyewe. Well done boys. Well done coach Moroco. Ndani ya mchezo ule Moroco na vijana wake wametuonyesha kwanini mchezaji wa timu ya taifa anajisikia...
EPL

Guardiola anapotuumbua wanafiki wake

Mbele ya hadhara Pep Guardiola ameamua kutuumbua wanafiki wake. Ametuumbua na kutuziba midomo kwa vitendo uwanjani sio kwenye ndimi kama sisi tulivyomuhukumu awali. Najisikia aibu kuwa mmoja wao. Pep na Manchester City yake wanafanya vyema. Pep mwenyewe haonekani kujali kwa maneno tuliyowahi kumkosoa nayo siku chache alivyotua uwanja wa Ndege...
CECAFA

Mudathir Yahya anapotupa maana ya mchezaji wa mkopo

Nimetazama Singida United. Nimeitazama Taifa Stars na sasa naitazama Zanzibar Heroes kule Kenya, kote huko namuona kijana mmoja wa kuitwa Mudathir Yahya akifanya kazi ya kiume katikati mwa uwanja. Mudathir anapokuwa katika ubora huu, ni ngumu kumzima. Aliwahi kuniambia moja ya rafiki zangu ambaye kesho anakutana uso kwa uso na...
Ligi Kuu

Mkwasa tusaidie ukweli wa Ngoma

KELELE za Donald Ngoma zimekuwa nyingi mitaa ya Jangwani. Dakika moja mwanachama huyu anazungumza hivi, dakika nyingine mwanachama yule anazungumza vile. Ngoma ndio ajenda kuu kwenye mazungumzo ya Yanga wakati huu. Kalamu yangu inayomalizia saa chache huku fungate nayo imeshitushwa na Ngoma. Mjadala wake umetikisa hadi makundi ya WhatsApp niliyoko....
Ligi

‘Nimemdhulumu mzee yule kwa toto hili’

SHABIKI mwandamizi wa Ajax Amsterdam, Mart Van Hoidonk mwaka 1996, alitoka uwanjani mpira ukiwa mapumziko na kuamua kurudi nyumbani. Rafiki yake aliyekuwa nyumbani alimshangaa Hoidonk aliyemuaga anakwenda uwanjani kutazama mpira, akirudi kabla mpira wenyewe kumalizika. Hoidonk kwa sauti yake ya chini alimwambia rafikiye kuwa asimshangae kurudi kabla ya mpira kumalizika...
1 3 4 5
Page 5 of 5