Ligi Kuu

GSM hawalipi mishahara YANGA – BUMBULI

Sambaza....

 

Baada ya kuwa na uvumi wa Yanga kutowalipa mishahara wachezaji wake , klabu hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ulitoa taarifa ya klabu kukanusha uvumi huo.

Baada ya kukanusha habari hiyo Afisa Habari wa klabu hiyo amedai kuwa mishahara ya klabu hiyo hailipwi na GSM, akizungumza na mtandao huu wa kandanda.co.tz amedai kuwa GSM hawalipi mishahara.

“Mishahara hailipwi na GSM , Mishahara inalipwa kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo klabu inavyo na siyo kwamba GSM ndiyo inalipa mishahara ya wachezaji”- alisema Afisa Habari huyo .

Kuhusu habari za kuwepo na wachezaji wanaolipwa na GSM na wengine kutolipwa na GSM , Afisa Habari huyo amekanusha uvumi huo .

“Hakuna mchezaji ambaye analipwa na GSM , na hakuna mgawanyiko wa kwamba kuna wachezaji wanaolipwa na GSM na wengine hawalipwi na GSM “- alimalizia Afisa Habari huyo


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.