Mataifa Afrika

Renard kuikacha Morocco baada ya AFCON.

Sambaza....

Vyombo mbalimbali vya habari nchini Morocco vimeripoti kwamba kocha wa timu ya Taifa Herve Renard anatarajia kuachia ngazi kuifundisha timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Mataifa Afrika.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia na Ivory Coast anatazamiwa kukitema kibarua chake baada ya kupata ofa nzuri kutoka kwenye timu inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa ya Olympique Lyon.

Inasemakana kwamba tayari Renard ameshafanya mazungumzo na Rais wa klabu ya Lyon Jean- Marc Aulas toka mwezi Januari na wameshakubaliana kujiunga nao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu nchini Ufaransa.

Renard ambaye aliisaidia Zambia kutwaa taji la AFCON mwaka 2012 kabla ya kuisaidia Ivory Coast nayo kutwaa ubingwa huo mwaka 2015 anarejea tena nchini Ufaransa alikozaliwa miaka 50 iliyopita kuendelea kuvifundisha vilabu vya huko, kwani alishawahi kuwa kocha wa Sochaux mwaka 2013-2014 pamoja na Lille mwaka 2015.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.