Sambaza....

Simba sc, imeisambaratisha Mbao FC kwa mabao 5-0 na kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, maarufu kama Vodacom Premier League

Mchezo huo uliofanyika kunako uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba walijipatia bao la kwanza kunako dakika ya 37, kupitia kwa Shiza Kichuya akimalizia kazi nzuri ya Emmanuel Okwi, dakika chache baadae Okwi aliipatia Simba bao la pili kwa njia ya penati baada ya mlinzi David Mwasa kumuangusha Okwi ndani ya eneo la hatari, hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa mabao hayo mawili.

TareheMwenyeji-Mgeni

Kipindi cha pili Simba sc, waliendelea kulisakama lango la Mbao FC kama nyuki na kunako dakika ya 68, Okwi aliipatia Simba bao la tatu baada ya kupokea pasi nzuri ya kiungo Mzamir Yasin aliyegongeana vema na Shiza Kichuya,

Simba waliendelea kutumia faida ya kutawala mchezo kwa asilimia kubwa kwa kusukuma mashambulizi ya mara kwa mara langoni kwa Mbao FC, na kunako dakika ya Erasto Nyoni aliiandikia Simba bao la 4 baada ya kupiga vizuri mpira wa kutenga nje kidogo ya eneo la 18.

Dakika ya 84, Mbao FC walilazimika kucheza wakiwa pungufu baada ya mlinzi na nahodha wake Yusuf Ndikumana kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya dhidi ya Laudit Mavugo.

Simba sc, walikamilisha karamu yao ya mabao kupitia kwa Nicholas Gyan aliyefunga kwa kichwa na kufanya hadi dakika 90, za mchezo huo zinakamilika Simba kuibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Ushindi huo unaifanya Simba sc kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha jumla ya alama 45, baada kushuka dimbani mara 19, huku mahasimu wa wakubwa Yanga sc, waliendelea kusalia kunako nafasi ya pili wakiwa na alama 37.

 

Sambaza....