Sambaza....

Nimeona video za wachezaji wawili wa Simba Sc Shomary Kapombe na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wakimwagika machozi baada ya kipigo cha mabao 5-1 dhidi ya mtani wao Yanga jana.

Nikaona na video za mashabiki wa Simba SC wakilalama mitandaoni kuhusu timu yao. Nimebaki kusimama kati. Machozi ya Tshabalala na Shomari yana majibu ya mashabiki wengi waliokuwa wanalalamikia wachezaji wao.

Shomary Kapombe

Shomari na mwenzake wanajua maana ya kupoteza dhidi ya mtani, tena kwa idadi kubwa ya mabao kama ile. Machozi yale sio ya kuigiza. Ni machozi yaliyotoka ndani ya mioyo yao.

Heshima, heshima, heshima. Baadhi ya mashabiki wa Simba SC wamewakosea heshima wachezaji wao.

Inauma kufungwa na mtani, lakini haipaswi kupitiliza mpaka kukosea watu adabu. Ndiyo maana kina Tshabalala wamemwagika machozi. Mashabiki walipaswa kusimamia pale katika yale machozi ya mastaa wao.

Mohamed Hussein.

Mara ngapi walimuona Shomari analia vile hadharani? Tena kilio cha kwikwi? Ni mara ngapi?

Simba SC wamepoteza mechi. Hawajapoteza matumaini ya kuwania makombe msimu huu. Mashabiki wasijitoe mchezoni kiurahisi. Japo inauma, lakini ni ngumu kusahau

 

Sambaza....