Shirikisho Afrika

Yanga Kumkosa Nabi Kesho, Kaze Atoa Ahadi Nzuri.

Sambaza....

Kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika Wananchi Yanga dhidi ya TP Mazembe watamkosa kocha wao mkuu Nasradine Nabi kwasababu za kifamilia.

Kesho benchi la ufundi la Yanga litakua chini ya kocha msaidizi Cedrick Kaze ambae amesema kila kitu kipo vizuri na wamejiandaa kupata matokeo mazuri.

 

Cedrick Kaze “Tumefanya mazoezi vizuri jana baada ya safari ndefu na leo pia tutapata nafasi nzuri ya kujiandaa na mchezo wa kesho, wachezaji wapo vizuri na naamini tutakua na mchezo mzuri pia kesho.

Kocha wetu Mkuu Nabi (Nasradinne) ataukosa mchezo wa kesho kwasababu za kifamilia. Mchezo huu ni muhimu sana kwetu kwasababi malengo yetu ni kumaliza vinara katika hatua hii ya makundi.” 

Nae nyota wa Yanga aliyehusika katika magoli mengi zaidi katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Kenedy Musonda amesema wanajua malengo yao wao kama wachezaji.

“Tumejiandaa vizuri na mchezo na tunajua nini malengo yetu katika mashindano haya makubwa na tupo hapa kwaajili ya kupambana na kuonyesha ukubwa wa Yanga Afrika,” alisema Kenedy Musonda

Yanga katika mchezo wao wa kesho pia watawakosa nyota wake watatu wa Kimataifa kutokana na sababu za nidhamu pamoja na usafiri. Djigui Diarra na Khalid Aucho watakosekana kwasababu wana kadi mbili za njano wakati Aziz Ki ameshindwa kupata usafiri wakufika Congo kutoka kwao alipokua akiitumikia Timu yake ya Taifa ya Burkina Faso.

Sambaza....