Sambaza....

Kiungo wa klabu ya Yanga, Ibrahim Ajib imeripotiwa kuna asilimia kubwa ya yeye kutocheza katika mchezo wa leo dhidi ya KMC.

Ibrahim Ajib amepata majeraha Jana akiwa mazoezini, na imeripotiwa majeraha hayo yanaweza kumsababisha Leo asiwepo kwenye mechi ya Leo.

Hili ni pigo kubwa sana kwa Yanga kumkosa Ibrahim Ajib katika mchezo wa Leo kwa sababu msimu huu amekuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi hicho cha wana Jangwani.

Mpaka sasa hivi amehusika katika magoli 11 kati ya magoli 14 ambapo Yanga imefunga. Hivo asilimia kubwa ya magoli ya Yanga yametoka katika mguu wa Ibrahim Ajib.

Sambaza....