Sambaza....

Wananchi Yanga watakua kibaruani ugenini dhidi ya Yanga katika mchezo wa raundi ya nane wa Ligi Kuu ya NBC katika Dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa kumi na moja jioni.

Wananchi wataingia uwanjani wakiwa kinara  katika msimamo wakiwa na alama 18 sawa na Watani wao Simba lakini Yanga wao wakiwa na wastani mzuri wa mabao yakufunga na kufungwa.

Dickson Job “Big Brain Defender”

Kuelekea mchezo huo mlinzi wa Yanga na Dickson Job ameongea kwa niaba ya wachezaji wenzake mbele ya Waandishi wa habari akiuzungumzia mchezo huo ukiwa ni miongoni mwa mechi mkubwa kwasasa Barani Afrika.

Akiongea katika mkutano huo Dickson Job alisema “Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho kwa Wanachama na Mashabiki wetu,” alisema Job maarufu kama “Big Brain Defender” na kuongeza;

“Tunajua nguvu yao (mashabiki) uwanjani wakija kutusapoti na tunawaomba kesho waje kwa wingi na kushangilia muda wote wa mchezo, kwa pamoja tuhakikishe tunaondoka na ushindi”

Miguel Gamondi.

Nae kocha wa Yanga raia wa Argentina Miguel Gamondi ambae anatoka Taifa hasimu na kocha Mbrazil wa Simba anaamini wanakwenda katika mchezo mzuri na anajua Afrika mzima inakwenda kutazama kandanda safi na la kuvitia.

Gamondi alisema “Utakuwa mchezo mzuri na wenye hisia, tumepata wiki nzuri ya maandalizi na tumefanya maandalizi mazuri. Wachezaji wako kwenye hali nzuri, Watanzania na Afrika kwa ujumla kesho watashuhudia mchezo bora.”

 

Sambaza....