Martin Kiyumbi

Mchambuzi
Mchambuzi wa mpira wa miguu, mwenye Shahada ya Ualimu. Martin amejiunga na timu ya kandanda toka mwaka 2017, moja kati ya wachambuzi wakongwe katika familia yetu.
Ligi Kuu

Sare ni kawaida , sisi ni mabingwa- BUMBULI

Jana Yanga walitoa sare nyingine ya nne mfululizo dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga . Sare ambayo imewaweka katika mazingira magumu ya kufukuzia ubingwa wa Tanzania Bara . Yanga mpaka sasa hivi wako nyuma ya alama 21 dhidi ya mabingwa watetezi Simba ambao ndiyo wanaoongoza msimamo...
Ligi Kuu

Yanga haina njaa , Simba watakufa tarehe 8- BUMBULI

Jana kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa na habari ambayo ilikuwa inazunguka kuhusiana na Yanga kushindwa kulipa mishahara yake . Yanga wamekanusha habari hiyo ambayo wamedai kuwa inawalenga kuwachafua wao kama wao pamoja na wadhamini wao GSM. Mtandao wa Kandanda.co.tz ulimtafuta Afisa Habari wa klabu hiyo Hassan Bumbuli ili kuzungumzia hili...
Ligi Kuu

GSM hawalipi mishahara YANGA – BUMBULI

  Baada ya kuwa na uvumi wa Yanga kutowalipa mishahara wachezaji wake , klabu hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ulitoa taarifa ya klabu kukanusha uvumi huo. Baada ya kukanusha habari hiyo Afisa Habari wa klabu hiyo amedai kuwa mishahara ya klabu hiyo hailipwi na GSM, akizungumza na mtandao huu...
Ligi Kuu

Nashusha bonge la mjengo Dodoma- ZAHERA

  Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera anataka kupafanya Tanzania kama nyumbani kwake baada ya Congo . Kocha huyo amedai kuwa ana mpango wa kujenga nyumba katika mji wa Dodoma ndiyo maana anatumia muda mwingi pia kuwepo Tanzania mara baada ya kuachana na Yanga . Kocha huyo...
Blog

Siondoki Tanzania mpaka YANGA wanilipe pesa zangu -ZAHERA

  Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera amekuwa akionekana sana hapa Tanzania kwa muda mrefu sana na kuzua maswali kwanini bado yupo Tanzania . Kocha huyo ambaye watu wengi walitegemea muda huu angekuwa na timu ambayo angekuwa anaifundisha Lakini amekuwa akionekana sana hapa nchini. Akizungumza na kituo...
Ligi Kuu

Nitarudi YANGA kama GSM wakiichukua YANGA -ZAHERA

  Kulikuwa na tetesi kuwa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga , Mwinyi Zahera anatakiwa tena na viongozi wa Yanga arudi kwenye kikosi hicho cha mabingwa wa Kihistoria. Akizungumza na kituo cha habari cha Global Online TV kuhusu uwezekano wa yeye kurudi Yanga siku moja amedai kuwa inawezekana...
Ligi Kuu

Mashabiki wa Yanga ni mamluki -NUGAZ

Moja ya vitu ambavyo mashabiki wa Yanga walikata tamaaa ni pale timu yao ilipopata suluhu dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Taifa. Suluhu ambayo iliwafanya wapate alama mbili katika michezo miwili iliyopita tena katika uwanja wao wa nyumbani wa Taifa jijini Dar es Salaam. Taratibu mioyo yao imeanza kukata...
Ligi Kuu

Yanga timu ya kawaida -KOCHA WA PRISONS

  Jana Tanzania Prisons waliwalazimisha Yanga Suluhu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam , uwanja ambao unatumiwa na Yanga kama uwanja wa nyumbani. Suluhu ambayo Yanga hawajafurahishwa nayo kutokana na mategemeo makubwa waliyokuwa nayo awali . Yanga katika mechi mbili zilizopita wamefanikiwa kupata alama mbili pekee. Tanzania Prisons...
1 2 3 65
Page 1 of 65
Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz