Abdul Mkeyenge

Mchambuzi
Mwandishi wa gazeti la Raia Mwema. Hapa anaandika makala za mpira wa ndani na nje.
tpl

Kisiga anaishi kijamaa katika dunia ya kibepari

Shaban Kisiga Malone. Mchezaji mmoja na nusu. Dead ball specialist. King of assist. Ball player. Ally Kamwe aliwahi kuniambia anachoweza kukifanya Said Juma Makapu kwa dakika moja, Kisiga anakifanya kwa sekunde mbili. Huyu ndiyo Kisiga aliyeamua kuukacha mpira na kukaa zake Vingunguti. Jumamosi asubuhi nilikuwa nikifuatilia mahojiane yake na kaka...
tpl

Wachezaji Simba wanafahamu thamani na uzito wa jezi wanazovaa?

LEO wacha nimtafune jongoo mbichi, bila kujali ukakasi nitakaoupata katika kinywa. Nina marafiki wengi ambao ni wachezaji wa Simba. Wao wananiheshimu kama Mwandishi nami nawaheshimu kama wachezaji. Lakini leo nimeamua kumtafuna jongoo, si vinginenyo. Simba imeshatua zake Dar es Salaam ikitokea Zanzibar kwenye Michuano ya Kombe la Mapinduzi. Imetua mchana...
epl

Liverpool wanapitia njia za ubingwa

Aliwahi kujisemea mwendawazimu mmoja kuwa shetani akizeeka anageuka Malaika. Rafiki zangu wa Liverpool zamani walikuwa wakiishi kishetani, lakini sasa wanaishi Kimalaika. Muda sio rafiki mzuri tena kwao. Zamani enzi za zama za mawe Liverpool walikuwa na kocha wao aliyekuwa akiitwa Bill Shanky. Shanky hakuwa kocha tu, alikuwa kama baba katika...
tpl

Simba imechelewa kumfukuza Omog

Ilianza kama tetesi. Ikaja kama uvumi. Hatimaye imekuja kuwa kweli. Simba imeachana na kocha wao Mcameroon Joseph Omog. Kila zuri na baya la Omog litabaki kwenye vitabu vyetu vya kumbukumbu. Binafsi naamini kuna kosa Simba imelifanya juu ya Omog. Kosa lenyewe ni kuchelewa kumfukuza. Nitakuelezea huko chini jinsi ilivyochelewa na...
tpluhamisho

Mgosi ‘again’? Naweka karata yangu kwake

MUSSA Hassan Mussa Mgosi amerudi tena uwanjani baada ya miezi kadhaa kujitokeza uwanja Taifa kulikokuwa kumetamalaki mashabiki wa Simba na kuchukua kipaza sauti na kusema ameamua kustahafu soka. Japo nilikuwa mbali na Mgosi alipokuwa akizungumza maneno yale, lakini alionekana kama mtu aliyestahafishwa sio kustahafu kwa matakwa yake. Alitoa chozi la...
epl

Moses amedhulumiwa jasho lake

NAPAZA sauti juu yangu nikisema wazi Victor Moses amedhulumiwa jasho lake. Nitasema hivi kokote kule ambako nitaitwa kuelezea amedhulumiwaje. Nitakueleza huko chini. Shusha pumzi kwanza. Haya ipandishe tuendelee. Jina la Moses haliko katika tatu bora ya wachezaji wa Afrika wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka huu. Majina yaliyoko ni...
mashindano

Heroes wametupa maana ya kuvaa jezi ya taifa

JANA jioni Zanzibar Heroes wamekufa kiume katika ardhi ya Mzee Jomo Kenyata pale Kenya. Wamekufa kiume kwa mapigo ya penati. Mapigo ya penati hayajawahi kuwa na mwenyewe. Well done boys. Well done coach Moroco. Ndani ya mchezo ule Moroco na vijana wake wametuonyesha kwanini mchezaji wa timu ya taifa anajisikia...
epl

Guardiola anapotuumbua wanafiki wake

Mbele ya hadhara Pep Guardiola ameamua kutuumbua wanafiki wake. Ametuumbua na kutuziba midomo kwa vitendo uwanjani sio kwenye ndimi kama sisi tulivyomuhukumu awali. Najisikia aibu kuwa mmoja wao. Pep na Manchester City yake wanafanya vyema. Pep mwenyewe haonekani kujali kwa maneno tuliyowahi kumkosoa nayo siku chache alivyotua uwanja wa Ndege...
CECAFA 2017

Mudathir Yahya anapotupa maana ya mchezaji wa mkopo

Nimetazama Singida United. Nimeitazama Taifa Stars na sasa naitazama Zanzibar Heroes kule Kenya, kote huko namuona kijana mmoja wa kuitwa Mudathir Yahya akifanya kazi ya kiume katikati mwa uwanja. Mudathir anapokuwa katika ubora huu, ni ngumu kumzima. Aliwahi kuniambia moja ya rafiki zangu ambaye kesho anakutana uso kwa uso na...
1 2
Page 1 of 2
Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz