Uhamisho

Andre Onana Hafai Kucheza Simba.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba imemtambulisha nyota wao mpya Willy Essomba Onana raia wa Cameroon ukiwa ndio usajili wao wakwanza kuutambulisha msimu huu.

Onana anajiunga na Simba akiwa mchezaji huyu baada ya kumaliza mkataba wake na wababe wa Rwanda APR ambako alimaliza Ligi ya Rwanda msimu uliopita akiwa mfungaji bora.

Kufuatia usajili huo kupitia kipindi chake cha michezo TBC Fm walifanya mahojiano na mwandishi wa habari kutoka Rwanda Clarise Uwimana na kutoa maoni yake kuhusu mchezaji huyo.

Willy Sambi Onana.

“Ni mchezaji mzuri alikuwa mfungaji bora licha ya kukosa mechi nyingi kwa sababu ya majeraha. Anaumia umia sana sijui kama itakuwa na athari gani kwa Simba.” Clarise Uwimana.

Mwanahabari huyo wa habari za michezo huyo kutoka Rwanda ameonyesha kushangazwa na usajili huo kwani anaamini wachezaji kutoka Rwanda sio daraja ambalo Simba wanapaswa kuwa nao.

“Ligi ya Rwanda iko chini Simba na Yanga ni timu kubwa sikutegemea kama wangesajiri mchezaji kutoka ligi ya chini zaidi kufananisha na ligi kuu ya Tanzania, nilitegemea wangeenda Morocco huko,” alisema Uwimana.


Sambaza....