Harambee vs Stars ni mechi ya ‘Afrika Mashariki’ na si mechi ya marudio ya zile nyingi ambazo wameshakutana, ni ‘vita’ , vita hasa ya kwenda kutengeneza rekodi mpya kwa kila timu kuvuka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.
Kumchezesha Msuva kama mshambulizi wa kwanza, Samatta akicheza nyuma yake itawapa walinzi wa Senegal wakati mgumu kiasi na kuwafanya wasiende sana kushambulia goli mwa Stars.