Mataifa Afrika

Amunike kweli alikutana na wababe

Sambaza....

Unaweza kusema kuwa Taifa na Harambee Stars zilipata vipigo halali kutoka kwa Algeria na Senegal katika kundi C. Timu hizi zote kila moja ilipata kipigo cha magoli matano katika mechi mbili (2+3), na kuzifanya ziage mapema kabisa katika michuano ya kombe la mtaifa ya Afrika nchini Misri.

Senegal na Algeria zilifuzu hatua ya nusu fainali, na sasa zote zinaingia fainali ya AFCON baada ya kuzitoa Tunisia na Nigeria.

Amunike

Kwa upande wa aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, anaweza akawa yeye kama yeye amechakazwa vibaya zaidi. Hii ni baada ya timu yake ya Taifa, Nigeria, kutolewa na timu ile ile ambayo ilipelekea yeye kutolewa mashindanoni na kupoteza kibarua chake.

Miamba ya soka hii barani Afrika sasa itakutana katika fainali hizo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.