
Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Kim Polsen ametaja kikosi kitakachoingia kambini kujiandaa na michuano ya kufuzu Afcon ya 2023.
Katika kikosi hicho hakina sura mpya sana wengi ni wachezaji walewale walioitwa katika michezo ya mwisho ya Kirafiki iliyopigwa nchini katika kalenda ya FIFA dhidi ya Afrika ya Kati.

Katika kikosi hicho wamejumuishwa Salum Abubakar na Himid Mao ambao walikosekana mda mrefu, lakini kwa upande wa John Bocco yeye ameendelea kukosekana na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwenzake wa Simba Kibu Denis.
Taifa Stars itaingia kambini May 28 mwaka huu kujiandaa na michezo miwili dhidi ya Niger June 4 ugenini na mchezo wa pili dhidi ya Algeria utakaopigwa June 8 Benjamin Mkapa.
Unaweza soma hizi pia..
Mambo sita yaliyoinyima alama Stars Kwa Mkapa!
blind passes) zilikuwa nyingi na madhara yake ikawa ni kupoteza umiliki wa mpira (possession) bila sababu ya msingi
Algeria wababe lakini kwa Mkapa hatoki mtu!
Dismas Kelvin John, Ben Stakie, Haji Mnoga na wengineo wakibadilishana uzoefu na nahodha Mbwana Samatta pamoja na Simon Msuva naamini hatuwezi kupoteza point zote 3.
Kocha Stars: Tuna kibarua kizito mbele ya Algeria!
Mchezo utakua mzuri tunacheza na timu ngumu lakini pia nasisi ni washindani hivyo haitakua rahisi na hautakua mchezo mwepesi.
Manara: Wachezaji wetu wamezoa mashabiki!
Kesho twendeni uwanjani tukashangilie timu yetu, hata kama itatokea bahati mbaya tumefungwa itakua ni sehemu ya mchezo maana wakati mwingine mpira una matokeo ya kikatili.