George Mpole
Tetesi

George Mpole Anarudi, Lomalisa Mambo Freshi.

Sambaza....

JKT Tanzania imeendelea kujiimarisha ili kutisha kwenye Ligi Kuu msimu ujao baada ya kupanda msimu huu ikitokea Championship ilikokuwa mabingwa na sasa imenasa saini ya beki wa kulia, George Aman Wawa kutoka Geita Gold ikimpa mkataba wa miaka miwili. [Mwanaspoti]

Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara, Msimu wa 2021/2022, George Mpole msimu ujao huenda akaendelea alipoishia baada ya Ligi Kuu DR Congo alikokuwa akicheza kwenye kikosi cha FC Lupopo kusimama kwa sababa za kiuchumi na vita na sasa yupo Bongo huku Geita Gold na Tabora United zikimpa ofa ya kutua katika vikosi vyao. [Mwanaspoti]

Klabu ya KMC inatajwa kukamilisha usajili wa mfungaji bora wa Kombe la FA (ASFC), Andrew Simchimba, aliyefunga mabao saba msimu uliopita akiwa na Ihefu [Mwanaspoti]

Joyce Lomalisa Mutambala (kulia) akimuacha mlinzi wa Tanzania Prisons.

BEKI wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa amekubali kubaki kuendelea kukipiga katika klabu hiyo hadi msimu ujao.Hiyo ikiwa ni siku chache tangu beki huyo kipenzi cha Yanga kutishia kuondoka klabuni hapo na kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine [Champion]

Pendekezo la Hakim Ziyech kuhama kutoka Chelsea kwenda Al Nassr limezimwa baada ya winga huyo wa Morocco, 30, kushindwa kufikia vigezo katika vipimo vya afya. [Mail]

Manchester United italazimika kuuza kabla ya kumnunua mlinda mlango wa Inter Milan raia wa Cameroon Andre Onana, 27. [Talksport]

Andre Onana

Nickson Kibabage tayari amemalizana na Yanga akitokea Singida Fountaine Gate na sasa anakwenda kuungana na Joyce Lomalisa katika eneo la ulinzi wa kushoto la Yanga.

Klabu ya JKT ipo katika mazungumzo na kiungo wa zamani wa Simba na Mtibwa Said Ndemla. Timu hiyo iliyopanda Ligi kuu imepania kujiimarisha ili kuleta upinzani haswa katika ligi ya msimu ujao.

 

 

Sambaza....