Sambaza....

Wananchi Yanga kesho Jumapili watashuka dimbani kuvaana na Asas Djibout majira ya saa moja usiku katik uwanja wa Azam  Complex.

Yanga wanacheza na Asas ya Djibout katika hatua ya awali ya Ligi ya mabingwa Afrika wakianza safari mapema ili kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

 

Kuelekea mchezo huo kocha wa Yanga Miguel Gamondi amesema”Tunakwenda kuiwakilisha Yanga na Tanzania kwa ujumla, naamini kesho tutakuwa na mchezo mzuri na kuwa na mwanzo mzuri kwenye Ligi ya Mabingwa,” alisema na kuongeza;

“Kitu muhimu zaidi kwenye mchezo ni kufunga magoli, tumejiandaa na tumelifanyia kazi hilo na ninaamini kesho mtaona mabadiliko makubwa kwenye eneo hilo,” alimalizia Gamondi.

Nickson Kibabage.

Nae ingizo jipya katika klabu hiyo Nickson Kibabage akiongea kwaniaba ya wachezaji wenzake ameseha hawatawadharau wapinzani na wapo tayari kwa mchezo.

“Hatudharau mpinzani, unapokutana na mpinzani kwenye Ligi ya Mabingwa bila shaka anakuwa amefanya vizuri alipotoka, tutakwenda kwa umakini mkubwa na kufanyia kazi yale ambayo kocha ametuelekeza,” Nickson Kibabage

Sambaza....