Ligi Kuu

Kauli ya Kwanza ya Mbeya City Baada ya Kushuka Daraja.

Sambaza....

Klabu ya Mbeya City imeshuka rasmi Ligi Kuu bara baada ya kudumu kwa miaka 10 tangu ilipopanda Ligi Kuu kwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya kufungwa na Mashujaa Fc ya Kigoma.

Mbeya City kupitia taarifa rasmi ya klabu baada ya kufungwa jumla ya mabao manne kwa moja na Mashujaa katika michezo yote miwili ilisema  “Asante sana Mbeya Jiji. Maneno ya mdomo hayawezi kueleza shukrani kwa fadhila mlizotuonesha leo; kuwa hata katika wakati mgumu mlikua nasi na kujaza uwanja wetu wa nyumbani, hatukua peke yetu.” 

Mbeya City ambao walipanda Ligi mwaka 2013 wamesema wao sio wageni wa Ligi daraja la kwanza (sasa Championship) huku wakisema wanawaachia Wanambeya maana mchezo wameuona wenyewe.

“Kuhusu mchezo, mmeuona, hauhitaji mtu mwenye masomo kuuchambua, tumeachana nao, na tunawashukuru ninyi mashabiki wetu kwa hamasa na uvumilivu wakati wote.

Tumecheza first division kwa misimu miwili 2011/12 na 2012/13, si kitu kigeni kwetu, tutaenda kucheza, na miaka 10 katika Ligi kuu imekua mizuri wakati wote, lakini mibaya leo hii. Tumejifunza, tutasahihisha makosa na kwa hakika —Tutarejea,” taarifa ilisema.

Sambaza....