Miguel Gamondi
Stori

Kocha Yanga: Hapa Tumepata Kipimo Halisi.

Sambaza....

Wananchi Yanga kesho watacheza na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika kuhitimisha kilele cha wiki ya Wananchi na kuelekea mchezo huo wa kirafiki kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ametema cheche.

Kuelekea mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa kocha huyo aliyechukua mikoba ya Nasraddine Nabi amesema “Kesho ni siku kubwa kwa mashabiki wa Young Africans SC pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania Klabu hii kubwa yenye historia kubwa” alisema Gamondi na kuongeza

“Kwenye upande wa timu bado tuko kwenye maandalizi na mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs na tutautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yetu kwa msimu ujao,” alimalizia kocha huyo Muargentina.

Benchi jipya la ufundi la Yanga.

Kwa mara ya kwanza kesho Jumamosi kocha Gamondi ataiongoza Yanga akiwa kama kocha mkuu baada ya kukipokea kibarua chake kipya mapema June mwaka huu.

Gamondi atapata kipimo halisi kutoka kwa Amakhosi ambao nao wamepania kufanya vyema msimu ujao baada ya kumaliza nje ya nne bora msimu uliomalizika.

Mashabiki wa Yanga pia watapa fursa ya kuwatazama wachezaji wao wapya siku ya kesho ikiwa sambamba na kuziona mbinu za kocha wao mpya.

Sambaza....