Fiston Kalala Mayele anatajwa kuhitajika na vilabu vya Uarabuni pamoja na Afrika Kusini
Tetesi

Kocha Yanga: Hatuna Uhakika Kama Mayele Atabaki Msimu Ujao

Sambaza....

Kufuatia kufanya vyema katika michuano ya ndani na nje ya nchi akiwa na Yanga mshambuliaji Fiston Mayele amekua lulu na kuhitajika na vilabu kadhaa vya nje ya nchi ikiwemo Afrika Kusini.

Kaizer Chiefs wanahusishwa na mshambuliaji huyo wa zamani wa Vita, ingawa hawakuonyesha kutuma ofa rasmi. Si tu Chiefs pia timu nyingine mbili za PSL zina nia ya kumnasa.

Kocha wa Yanga, Nabi amefichua kuwa hana uhakika kama watabaki na mshambuliaji wao huyo bora. Katika misimu yake miwili Yanga, Mayele amefunga mabao 52 katika michuano yote. “Ndiyo, ninamfurahia sana kwa sababu mimi ndiye niliyemgundua kutoka AS Vita na kumleta kwenye timu. Bado mwaka mmoja kwenye mkataba wake umalizike. Hatuna uhakika kama atasalia kwa sababu kuna timu zinamuhita kutoka duniani kote,” aliiambia FAR Sports na kuongeza

Fiston Kalala Mayele

“Hatujui tutachezaje bila yeye msimu ujao, lakini ndivyo ilivyo.”

Kwa sasa Mayele ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa amefunga  mabao 16. Katika msimu wake wa kwanza, alifunga mabao 16, akikosa tuzo ya mfungaji bora kwa bao moja tu. George Mpole wa Geita Gold alishinda tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 17 kabla ya kuhamia FC Lupopo ya Congo mwanzoni mwa msimu.

Sambaza....