Alli Kamwe msemaji wa klabu ya Yanga
Shirikisho Afrika

Msemaji Yanga: Kila Mtu Anatakiwa Kuisaidia Yanga Kupata Ushindi

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Rivers United dhidi ya Yanga msemaji wa klabu ya Yanga Alli Kamwe ameongea na waandishi wa habari na kutoa rai kwa mashabiki wote wa Yanga.

Alli Kamwe amewaambia wapenzi na mashabiki wote wa klabu ya Yanga kila mmoja ana jukumu la kuisaidia Yanga ipate matoekea mazuri na si tu uongozi ama benchi la ufundi ndio wana hilo jukumu.

“Jukumu la kupata ushindi katika mchezo wa ugenini dhidi ya Rivers United ni la watu wote, sio la Nasradine Nabi na benchi lake la ufundi, sio jukumu la Rais Hersi Said au Makamu wa Rais Arafat Hajji pekee,” alisema Alli Kamwe na kuongeza

Mashabiki wa Wananchi Yanga.

“Kama uongozi una nafasi yake katika kufanikisha ushindi katika mchezo huo lakini  pia nanyinyi mashabiki na wapenzi wa Klabu ya Yanga mna nafasi yenu tena kubwa tuu katika kuisaidia timu kupata ushindi.”

Yanga watasafiri kuelekea nchini Nigeria katika mchezo wa kwanza dhidi ya Rivers na tayari kikosi kipo kambini kwaajili ya maandalizi na tayari wameshaweka utaratibu pindi ambapo timu itakapowasili nchini Nigeria kuelekea mchezo huo mgumu.

Alli Kamwe “Tayari Nimeshawaambia  na kuwaelezea jinsi ambavyo maandalizi na kambi itakavyokua kule nchini Nigeria. Yanga inabidi tuungane tuwe wamoja katika michezo hii miwili, hivyo hata kama kuna mtu anataka kupiga dua kwaajili ya kuiombea Yanga wafanye tuu hakuna shida yoyote.

Rivers United wapinzani wa Yanga

Na jukumu hili ni la watu wote mara nyingi mashabiki waliopo nje ya Dar es salaam wamekua wakiona hili jukumu ni la watu wa Dar pekee hapana, kuanzia leo viongozi wa matawi Dodoma, Chalinze, Mbeya mkutane muweke kikao ni jinsi gani Yanga itapata ushindi,” alimalizia Alli Kamwe.

Kikosi cha Yanga kinategemewa kuanza safari ya kuondoka nchini kesho alfajiri kuelekea nchini Nigeria wakipitia nchini Ethiopia. Mchezo huo utapigwa kusini mwa Nigeria katika Jimbo la Akwa Ibom

Sambaza....