Uhamisho

Mshambuliaji Simba akimbia benchi, katimkia Ihefu

Sambaza....

Mshambuliaji kinda wa klabu ya Simba Cypriani Kipenye ameondoka katika klabu yake ya Simba na kwenda kujiunga na Ihefu fc ya jijini Mbeya.

Kipenye ambae ni zao la Simba B ambapo alipandishwa katika msimu uliopita na mwalimu Sven baada ya kumvutia sasa anakwenda kuungana na “walima mpunga” Ihefu fc kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja.

Uwepo wa washambuliaji wazoefu Meddie Kagere na John Bocco lakini pia maingizo mapya Cris Mugalu na Charles Ilanfia kumemfanya Kipenye kutafuta mahala pengine ili kuweza kulishawishi benchi la ufundi kuliko kukaa benchi Simba.

Kipenye alianza vizuri katika michezo ya kujiandaa na msimu ambapo alifunga mabao mawili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Campu katika uwanja wa Uhuru.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.