Uhamisho

Mshambuliaji Simba atimkia Uturuki.

Sambaza....

Nyota wa timu ya Simba Queens vinara wa ligi ya wanawake na timu ya Taifa ya Tanzania kwa upande wa wanawake ameondoka nchini na kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Uturuki.

Opa Clement aliekua nahodha wa Simba Queens amejiunga na Besiktas ya Uturuki inayoshiriki Ligi kuu ya wanawake nchini humo.

 

Nyota huyo wa Simba si mara ya kwanza kwenda Ulaya kwani awali alikwenda huko muda mfupi lakini alirudi baada ya mambo kutokukaa sawa.

Uongozi wa Simba umemtakia kila lakheri nahodha wake huyo aliyeiacha timu ikiwa kileleni baada ya michezo ya raundi ya awali kumalizika.

Opa Clement.

Opa aliiongoza timu yake ya Simba Queens kufika nusu fainali ya Ligi ya mabingwa ya wanawake Afrika waliposhiriki kwa mara ya kwanza msimu uliopita.

Sambaza....