Sambaza....

Novatus Dismas Miroshi atakuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mashindano ya Ligi ya mabigwa barani Ulaya msimu ujao.

Hujakosea kusoma wala hauko ndotoni. Ni kweli Novatus Dismas atacheza mashindano hayo. Huu ni ushindi kwa kijana wa Kitanzania kuziaminisha ndoto zake na ndoto za vijana wengine waliozaliwa na kukulia katika mazingira magumu.

 

Tulihitaji taarifa za namna hii ili kuwaamsha vijana wengine waliojikatia tamaa. Kwangu hii ni taarifa nzuri. Ni taarifa inayokwenda kuuambia Moyo wangu kuwa inawezekana, bila kujali unapitia magumu na machungu mangapi katika maisha.

Keep it up Novatus. Keep it up Shadaka Sports Agency kwa kuendelea kuwafungulia dunia vijana wa Kitanzania kuwa wanachokitaka.

Novatus hapo awali alipitia klabu ya Azam Fc ambao walimtoa kwa mkopo kwenda Biashara United na kuibuka mchezaji bora chipukizi na hapo ndio maisha yake ya soka yakaanza kubadilika.

Novatus Dismas Miroshi.

Baadae Nova alijiunga na Makabi Tel Aviv akianzia timu ya vijana kabla ya kupandishwa na wakamuuza Ubelgiji katika klabu ya Zulte Waregem.

Akiwa na thamani ya Euro laki saba. (€700 k) sasa Novatua anatajwa kuelekea katika klabu ya Shakhter Donetsk ya nchini Ukraine.

Sambaza....