Nasraddine Nabi akiwa na mashabiki wa Yanga.
Stori

Nabi Nasraddine Ndani ya Kitabu cha Kumbukumbu Yanga!

Sambaza....

Miaka 30 iliyopita Yanga imekuwa na bahati yakuwa na makocha bora ambao kwa nyakati tofauti wameandika historia zao maridhawa na klabu hii kongwe zaidi nchini .

Mitaa ya Jangwani amepita mwamba Tito Mwaluvanda akiwa msimamizi tu wa mazoezi Yanga ikatinga hatua ya makundi klabu bingwa Afrika mwaka 1998 . Pumzika kwa amani kocha.

Raoul Shungu na kikosi cha dhahabu hakuna wa kumsahau mitaa ya Jangwani . Aliifanya Yanga kuwa imara akiipa vikombe na heshima ukanda wa CECAFA.

Tambwe Leya 1994 anaisuka Yanga yosso na kutetea ubingwa wake Khartoum Sudan (Kagame Cup) . Huyu anakumbukwa kwa soka safi na misimamo yake akiacha kauli ya kishujaa na kiutendaji kwa benchi la ufundi . “ ukitaka kufanikiwa ni lazima wachezaji wako na viongozi watambue wewe ndio BOSS wa timu “ . Pumzika kwa Amani Tambwe Leya .

Hans Van Plujim.

Van Pluijm aliisuka Yanga ya kampa kampa tena kiasi cha kuwapoteza wapinzani wao Simba katika ubingwa wa ligi kwa misimu mitano. Pluijm ambaye kwa sasa ni kocha wa Singida ana alama yake pale Jangwani.

Nabi amepita njia ile ile ambayo watangulizi wake wamepita na kupiga hatua nyingi mbele . Ameigeuza Yanga kuwa timu tishio nchini na Afrika kwa ujumla . Historia yakuwa “unbeaten” kwa mechi 49 , nusu fainali Shirikisho Afrika na ubingwa mfululizo wa ligi kuu pia FA .

Nabi anaitendea haki kauli ya marehemu Tambwe Leya “ ni Boss wa timu “ . Hersi na uongozi wake wanaitambua nafasi ya kocha wao na wachezaji pia kiasi kila mmoja katika klabu anampa heshima yake na yeye anawapa matunda ya kazi yake .

Nasraddine Nabi.

Si mapema kukubali kuwa Nabi ni bora na anaweza kuitanua zaidi ramani ya Yanga ndani ya Afrika.
Hongera kwa ubingwa!!

Samweli Samweli.

Sambaza....