EPL

Pochettino afungiwa mechi mbili

Sambaza....

Chama cha soka nchini Uingeleza(FA) kimfungia kocha wa Tottenham mechi mbili kufuatia kitendo cha kurumbana na mwamuzi Mike Dean

Mauricio Pochettino, amepewa adhabu hiyo na FA ya kutoiongoza timu yake katika michezo miwili kufuatia kutoelewana na mwamuzi Mike Dean baada ya timu yake kupoteza kwa Burnley mwezi uliopita

Meneja huyo wa Spurs, aliomba msamaha kwa kitendo hicho “Nimeona tabia yangu baada ya kutazama kwenye Tv, nafikiri natakiwa kukubari na kuomba msamaha kwa Mike Dean. Siwezi kuwa vile, sio njia”

“Tabia yangu kwa jamii na kwa sasa natakiwa kuiomba msamaha, nahitaji kuomba msamaha kwake na maofisa wote” aliongeza kocha huyo

Pochettino, pia atatakiwa kulipa faini ya paundi 10,000 na kufungiwa kwake kutamfanya akose mchezo wa ugenini dhidi ya Southampton na ule wa nyumbani watakaoikaribisha Crystal Palace


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.